Back to top

SERIKALI KUDHIBITI UVUJAJI WA MITIHANI

05 July 2023
Share

Serikali imesema inaendelea kudhibiti uvujaji wa mitihani na kuchukua hatua kwa wanaobainika kuhusika na vitendo hivyo, vinavyoathiri ukuaji wa sekta ya elimu kwa kusababisha kupatikana kwa wataalam wasiokuwa na viwango vinavyohitajika.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda, ametoa kauli hiyo Jijini Mwanza, wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo maofisa elimu kata kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Amesema vitendo vya wizi wa mitihani vimekuwa vikiwanyima haki wanafunzi wengine lakini pia wanafunzi wanaofanya udanganyifu wanapelekea taifa kuwa na wataalamu wasiokuwa na weledi ambao wanasaababisha utekelezaji wa miradi chini ya kiwango.

Kwa upande wao, maofisa elimu hao wanaojengewa uwezo kuhusu matumizi yaTeknolojia na Habari na Mawasiliano (TEHAMA) hasa vishkwambi wamesema itawasaidia kupunguza gharama za kusafirisha makaratasi ya tarifa kutoka shule mbalimbali na utunzaji wa nyaraka za serikali kirahisi.