Back to top

Serikali kudumisha amani kama siri ya maendeleo

14 April 2022
Share

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema Serikali itaendelea kudumisha amani, mshikamano na utulivu kama siri ya mafanikio ya maendeleo na ustawi wa watanzania wote pamoja na kuhakikisha shughuli za uzalishaji zinafanyika katika mazingira salama ambapo pia amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujenga uhusiano na ushirikiano na mataifa mengine Duniani na namna anavyosaidia kuitangaza Nchi kimataifa.