
Serikali imesema inaendelea kutekeleza na kutokomeza ukatili wa kijinsia kupitia mpango unaotekeleza mambo kadhaa yakiwemo ya usawa wa kijinsia na kuweka frusa sawa kwa Watanzania.
Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, wakati akizindua mpango wa haki za wanawake unaolenga utokomezaji wa ukatiri wa kijinsia.

Sehemu nyingine ambayo ripoti imehimiza ni kuweka mfumo bora wa usawa kwa wote na kama tulivyoona athari za mlipuko wa corona ulivyoleta athari katika suala la ajira kwa wanawake, hivyo ni muhimu utekelezwaji wa mikakati kama hiyo ikafanyika kuchochea mfumo bora wa ulinzi kwa jinsia zote jambo litakalosaidia kuwainua kiuchumi wanawake.
Canada inaungana katika utekelezwaji wa mpango huu ili kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na usawa pande zote kwa wanaume na wanawake ili kuchochea ukuaji wa fursa za kiuchumi pande zote, kupitia fursa zinazojitokeza.

