Back to top

Serikali kufanya tathimini ya maeneo yaliyopteza sifa kuwa hifadhi.

02 May 2018
Share

Serikali kupitia wizara ya Maliasili na utalii imepanga kufanya tathimini ya maeneo yaliyopoteza sifa kwa kushirikiana na taasisi ya utafiti wa wanyama pori Tanzania-TAWIRI - ili kubaini yaliyopteza sifa za kuendelea kuwa hifadhi na kuyaondolea hadhi ya uhifadhi ili yatumike ipasavyo kwa shughuli za kilimo ma ufugaji.

Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Japhet Hasunga akijibu swali la mbunge wa Biharamulo Magharibi Mheshimiwa Oscar Mukasa Serikali imeshaanza kuandaa moango wa kuyaondolea hadhi baadhi ya maeneo ya hifadhi kwa kuwa yamepoteza sifa.

Mheshimiwa Hasunga amesema baada ya tathimini kukamilika, serikali itaanda mpango ambao utahusisha wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi na halamshauri za wilaya ili kuhakikisha kuwa maeneo yatakayo ondolewa hadhi ya uhifadhi yanatumika ipasavyo.

Amesema maeneo ya hifadhi yameanza na kutangazwa kisheria kwa kuzingatia umuhimu wake kiikolojia, kiuchumi, kiusalama na kijamii kwa Maslahi ya Taifa, aidha baadhi ya maeneo hayo yanakabiliwa na tatizo la uvamizi unaotokana na shughuli za kibinadamu kama kilimo na mifugo.