Back to top

SERIKALI KUJENGA UPYA SHULE YA SEKONDARI KENGEJA.

02 February 2024
Share

Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameahidi kujenga upya Shule ya Sekondari Kengeja  pamoja na bweni la wavulana lililoungua moto.


Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipotembelea Bweni la wavulana  katika Shule ya Sekondari Kengeja, ambalo limeungua moto usiku wa Januari 31, 2024, Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba. 

Rais mwili ametembelea shule hiyo baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Pemba na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe.Mattar Zahor Masoud na viongozi mbalimbali na ameshukuru makampuni, wadau mbalimbali waliojitokeza na kuchangia misaada mbalimbali kwa ajili ya shule hiyo.

Naye, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Lela Mohamed Mussa amewashukuru wadau mbalimbali waliojitolea michango akiwemo msamaria mwema aliyejitolea shilingi milioni 300, mfanyabiashara Rostam Aziz milioni 100, benki ya NMB wametoa magodoro 70 na mashuka 70, ZRA shilingi milioni 5, kampuni ya Vigor Group shilingi milioni 5, mfanyabiashara Hussein Muzzamil shilingi milioni 1,  pamoja na KOICA wametoa sare za shule za wanafunzi 70.