
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Abdallah Ulega amesema Wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani inaweka mikakati imara ya namna ya kukabiliana na matukio ya uvamizi wanayofanyiwa wavuvi na watu wanaodaiwa kutoka nchi jirani na kuwanyang'anya vifaa vyao vya kazi na wakati mwingine kuhatarisha maisha yao wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao ndani ya Ziwa Victoria.
.
Ulega ametoa kauli hiyo katika Mwalo wa Makoko uliopo katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maswala ya Ukimwi, Kifua kikuu, Madawa ya Kulevya na Magonjwa yasiyoambukiza kutembelea katika mwalo huo.
