Back to top

Serikali kulifanyika kazi swala la likizo ya uzazi kwa watoto njiti.

30 April 2018
Share

Serikali imepanga kulifanyika kazi swala la kuwaongezea muda wa likizo ya uzazi wa watoto njiti kuwa miezi sita pamoja na malipo kwa mujibu wa mwongozo wa kanuni za utumishi wa umma.

Akijibu swali la Mbunge wa Ileje Mheshimiwa Janeth Zebedayo Mbene aliyeuliza serikali haioni ni muda mwafaka wa kuwaongezea muda wa likizo ya uzazi,wazazi wa watoto njiti kuwa miezi sita pamoja na malipo pamoja na serikali inamkakati gani wa kuhakikisha vifaa vya kuhudumia watoto njiti vinapatikana katika hospitali za wilaya ya .

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI- Mhe Seleman Jafo amesema Halmashauri ya wilaya ya Ileje imetenga shilingi milioni 12 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kuhusumia watoto njiti.

Amesema katika mkoa wa Songwe kwa mwaka 2018/19 zimetengwa shilingi Milioni 22.1 kwa ajili ya utoaji wa mafunzo maalum ya kuaidia mtoto njiti,aidha amesema katika ngazi ya hospitali kuna mashine 3 za kusaidia kupumua pamoja vifaa vya kusaidia watoto wachanga kupumua vipi katika ngazi ya zahanati,afya na hospitali.