Back to top

SERIKALI KUMALIZA CHANGAMOTO ZA MAFURIKO RUFIJI NA KIBITI

12 April 2024
Share


Serikali imesema itamaliza changamoto ya mafuriko katika wilaya ya Rufiji na Kibiti  kwa kujenga mabwawa makubwa mawili katika kata ya Ngorongo tarafa ya Mkongo na eneo la Kitunda wilaya ya Kibiti kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI Mhe.Mohammed Mchengerwa amesema hayo Rufiji baada ya kupokea misaada mbalimbali vikiwemo vyakula na fedha za kununulia mbegu iliyotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili ya waathiriwa wa mafuriko.

Naye Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Abdallah Ulega amesema serikali itatoa boti itakayosaidia usafiri na shughuli za uokozi.

Baadhi ya taasisi za nje ya wilaya hizo zimejitokeza kutoa misaadambalimbali kwa waathirika wa mafuriko.