Back to top

SERIKALI KUREJESHA TENA MAONESHO YA NANE NANE

31 May 2022
Share

Serikali imeliambia bunge kuwa imeamua kuyarejesha tena maonesho ya nane nane baada ya maonesho hayo kusimama kwa takribani miaka miwili.

Waziri wa Kilimo Mhe.Husein Bashe amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Singida Mhe.Rita Kabati  aliyetaka kujua hatma ya maonesho hayo.

Waziri Bashe amesema kuanzia mwaka huu maonesho hayo yatasimamiwa na Serikali na siyo taasisi ya TASO kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Maonesho hayo ya nane nane hufanyika kikanda lengo likiwa ni kuwapa wakulima mbinu za kisasa za kilimo na jinsi ya kutafuta masoko ya mazao yao.