Back to top

Serikali kutekeza mradi wa umeme, Rumakali

31 July 2022
Share

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amefika kwenye mradi wa kufua umeme kwa njia ya maji wa Rumakali (MW 222) wenye thamani ya Shilingi Trilioni 1.4 uliosanifiwa tangu mwaka 1998, ambapo amebainisha kuwa serikali imeamua kuutekeleza mradi huo uliopo wilayani Makete mkoani Njombe ili kuwezesha nchi kuwa na Umeme wa kutosha, na kuanzia Agosti 01, 2022 wathamini watafika kuzungumza na wananchi kuhusu fidia za maeneo yatakayochukuliwa.
.
Mhe.Makamba ameyasema hayo akiwa katika ziara yake wilayani humo.