Back to top

Serikali kutoa huduma bora Idara ya Ustawi wa Jamii.

24 November 2021
Share

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Dorothy Gwajima amesema kuwa Serikali imejipanga  kuendelea kuboresha na kusimamia utoaji huduma bora kwa jamii kupitia idara ya ustawi wa jamii kwa lengo la kupunguza changamoto eneo hili zikiwemo wimbi la watoto wa wanaoishi kwenye mazingira magumu na hatarishi pia na wale wanaokinzana na sheria. 

Dkt.Gwajima  amebainisha hayo katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Wataalamu na Watoa Huduma za Ustawi wa Jamii ( TASWO ) na Kongamano la Kitaifa Tanzania Bara na Visiwani lililofanyika  jijini Mwanza.

Dk Gwajima amesema tayari Wizara imekamilisha kufanya mapitio ya Sera ya Wazee ya mwaka 2003 na kuandaa andiko la wasilisho serikalini kwenye Baraza la Mawaziri kwa hatua zaidi.

Amesema Serikali imeendelea kufanya utambuzi wa kaya masikini na kutoa bima za afya na matibabu bila malipo kwa wazee tangu mwaka 2015.