Back to top

Serikali kutoa mikopo kupitia mfuko wa pembejeo kukopesha wakulima.

17 April 2018
Share

Serikali imesema itaendelea kutoa mikopo kupitia mfuko wa pembejeo lengo ikiwa ni kukopesha wakulima pembejeo na zana za kilimo kwa gharama nafuu na riba yake ikipunguzwa hadi kufikia asilimia sita.

Kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na 2017/2018 mfuko wa pembejeo umekwisha kutoa mikopo yenye thamani ya Shilingi Milioni 789 kwa wakulima wa mikoa ya Singida na Dodoma mikopo iliyojumuisha matrekta, pembejeo za kilimo, nyenzo za umwagiliaji na usindikaji.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo, Dakta. MARRY MWANJELWA alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki Mheshimiwa ALLAN KIULA aliyetaka kujua ni lini serikali itachukua hatua za makusudi kutenga mitaji kwa wakulima kupitia benki za mikopo.

Hadi kufikia Machi mwaka huu Benki ya kilimo nchini ilikuwa imekwisha idhinisha mikopo ya Shilingi Bilioni 38, kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kilimo nchini.