Back to top

SERIKALI KUTOONGEZA MUDA MKATABA WA SONGAS

18 May 2022
Share

Serikali imesema haitaongeza muda wa mkataba wa Songas pindi utakapoishia Mwezi Julai, 2024 badala yake itajadili mkataba mpya na  iwapo pande zote zitakubaliana, mkataba mpya wenye tija kwa Taifa na usio kuwa na dosari ndio utakaosainiwa. 

Kauli hiyo imetolewa Bungeni Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Stephen Byabyato wakati akijibu swali la Jesca Kishoa, Mbunge wa  viti maalum. 

Mbunge huyo alitaka kujua Serikali imejipangaje kuhakikisha Mkataba mpya wa Songas usiokua na dosari na kwa manufaa ya Wananchi  utakapoishia mwaka 2024 utafanyikaje ili kupata mkataba wenye tija.

Akaongeza kuwa mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya Songas utaisha muda wake Mwezi Julai, 2024 Serikali haitaongeza muda wa mkataba  utakaoishia Mwezi Julai, 2024.

MhE. Byabato akasema Serikali itajadili mkataba mpya na iwapo pande zote zitakubaliana, mkataba mpya wenye tija kwa Taifa na usio kuwa na dosari utasainiwa.

Naibu huyo akaeleza kuwa tayari Serikali kupitia TANESCO imeunda Timu ya kupitia masuala ya msingi ya kuzingatiwa kwenye mkataba mpya  kwa ajili ya maslahi kwa Taifa.