Back to top

Serikali kuwajengea ujuzi wa kutosha wahitimu

02 June 2022
Share

Serikali imesema katika mageuzi ya elimu yanayofanywa nchini imekusudia kuwajengea ujuzi wa kutosha wahitimu ili kuwarahisishia kuweza kuingia katika soko la ajira ili waweze kuajiriwa au kujiajiri pasina kupoteza ubora wa elimu.
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe.Didie Chassot ofisini kwake Jijini Dodoma.
.
Aidha Waziri Mkenda amesema kuwa ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili hususani katika maeneo ya kuongeza ujuzi kwa vijana na kuimarisha upatikanaji wa ajira pamoja na vyuo vya ufundi utaendelea ili kuhakikisha kuwa nchi hizo mbili zinaimarika na kuwa na weledi mkubwa katika sekta ya elimu.