
Waziri wa nchi sera,ajira, uratibu na Bunge Mheshimiwa Jenista Mhagama amesema kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wazalendo na wageni ili kuinua uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi katika kijiji cha Maniamba wilayani Songea mkoani Ruvuma katika mkutano wa hadhara uliouhuduriwa na mwekazaji kutoka China na mwekezaji wa kampuni ya kizalendo ya Kamba's Group inayochimba makaa ya Mawe katika kijiji hicho.
Katika mkutano huo kampuni ya Kamba's Group imetoa Bati,Nondo,Misumari na Saruji kwa ajili ya kukamilisha ofisi ya kijiji cha Maniamba ambapo kwa sasa wanatumia jengo la mashine ya kusaga nafaka kama ofisi.