
Serikali imesema itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kuifanya sekta binafsi iweze kujenga viwanda vipya kadri inavyowezekana.
Waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji Charles Mwijage amesema hayo bungeni mkoani Dodoma wakati akijibu maswali ambayo yalielekezwa kwa wizara yake.
Amesema katika kutekeleza hilo Serikali na sekta binafsi wamekuwa wakikutana mara kwa mara ili kuweza kujadiliana na jinsi ya utekelezaji wa hilo.
Wabunge pia walielezwa kuwa kasi ya ujenzi wa viwanda mia moja katika kila mkoa ndani ya mwaka mmoja inaenda vizuri.