Back to top

Serikali kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji.

11 September 2019
Share

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Ashatu Kijaji amesema serikali kwa sasa imejielekeza katika kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na kufanya biashara kwa kutumia ongezeko la watu kama fursa ya nguvu kazi ya kuzalisha mali pamoja na soko la bidhaa na huduma.

Mhe.Kijaji ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mhe. Boniface Getere Mbunge wa Bunda vijiji aliyeuliza upi mkakati wa serikali kutumia au kudhibiti kasi ya idadi ya watu nchini.
 
Mhe.Kijaji amesema utafiti wa wa idadi ya watu duniani unaonesha idadi kubwa ya watu ni fursa kwa nchi iwapo baadhi ya mambo matano yatafanyika.

Amesema miradi mingi inayoendelea nchini kwa sasa inalenga kufungamanisha fursa za kiuchumi na ongezeko la idadi ya watu na jitihada hiyo zinarandana na mambo yalipendekezwa kwenye ripoti ya utafiti wa idadi ya watu duniani na athari zake.