Back to top

Serikali: Marufuku wananchi kusainishwa mikataba kwa lugha za kigeni.

21 July 2021
Share

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew amepiga marufuku kwa makampuni ya simu nchini kuwasainisha wananchi mikataba kwa lugha za kigeni, kwa sababu yeyote anayefanya hivyo lazima kutakuwa na dhamira ovu dhidi ya wananchi ndio maana anawasainisha mikataba kwa lugha wasiyo ifahamu.
.
Naibu Waziri Kundo ameyasema hayo akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi, uwezo na ubora wa minara ya mawasiliano katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga ambapo alitembelea mradi wa ujenzi wa mnara uliopo katika Kijiji cha Tanga B na kumhoji mmiliki wa eneo hilo ambaye alisema kuwa alisaini mkataba wa makubaliano ya awali ya kufanya ujenzi katika eneo lake uliokuwa umeandikwa kwa lugha ya Kiingereza na Kivietinamu.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew (wa tatu Kulia
mstari wa mbele) akifuatiwa na Mbunge wa Muheza Mhe. Hamis Mwinjuma wakisikiliza maelezo
ya Mradi wa Ujenzi wa mnara wa mawasiliano.