Back to top

Serikali mkoa wa Kilimajaro yakiri kuonekana Nzige.

11 February 2020
Share

Serikali Mkoani Kilimanjaro imesema, Nzige wameonekana katika baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Moshi.

Mkuu wa mkoa huo,Dkt.Anna Mghwira amesema wakati wa asubuhi wadudu hao walikuwa hawajaonekana, lakini kwenye majira ya jioni walionekana katika baadhi ya vijiji.

Amesema jana alizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Taveta nchini Kenya ambaye naye alimthibitishia kutokuwepo kwa wadudu hao hata katika wilaya za jirani.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Kilimanjaro , Bwana Patrck Boisafi ameiomba Serikali ichukue hatua ya kupambana na wadudu hao kwa kuwa madhara yake ni ma kubwa ikiwemo njaa na kuyumba kwa uchumi katika taifa na katika jamii.