Back to top

Serikali: Msiwachangishe fedha wananchi.

23 November 2021
Share

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Ummy Mwalimu amepiga marufuku wananchi kuachangishwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa yanayojengwa na fedha zilizotolewa kwa ajili ya UVIKO 19. 


Waziri Ummy amepiga marufuku hiyo wakati akiendelea na ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mkoani Iringa ambapo amefafanua kuwa serikali haiwazuii wananchi kuchangia nguvu kazi kwa kuwa wamekuwa wakijitoa katika kutekeleza miradi ya maendeleo ili kuunga mkono juhudi za Serikali.