Back to top

Serikali ya Zambia kuhimiza mageuzi ya kisiasa na kisheria.

22 January 2020
Share

Rais Edgar Lungu wa Zambia amesema serikali yake itaendelea kuhimiza mageuzi ya kisiasa na kisheria yanayolenga kuhakikisha maendeleo endelevu ya biashara ndogondogo na ya katikati.

Amesema utafiti umeonesha kuwa sekta hiyo imekuwa na uwezo wa kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi na utoaji wa nafasi za ajira.

Rais Lungu amesema, kwenye upande wa utoaji wa nafasi za ajira, ili kuziwezesha biashara ndogondogo na zenye ukubwa wa kati kutoa nafasi za ajira na kutoa mchango mkubwa zaidi katika ukuaji wa uchumi, kutakuwa na sera nzuri na mfumo wa kisheria kuhimiza sekta hiyo.

Ameongeza kuwa serikali hiyo itaendelea kutekeleza mageuzi muhimu kushughulikia leseni na sheria za makampuni, usafirishaji wa biashara na urahisishaji wa kufanya biashara, ili kuhimiza ukuaji wa biashara ndogondogo.