Back to top

SERIKALI YADHIBITI KUENEA VIRUSI VYA MARBURG

25 March 2023
Share

Serikali imesema imefanikiwa kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya homa ya ugonjwa wa marburg , uli ozuka mkoani Kagera, kata za Maruku na Kanyangereko  na kusababisha vifo vya watu watano na wengine watatu wanaendelea kutibiwa ugonjwa huo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya ,Mh. Ummy Mwalimu,  alipozungumza na wanahabari mjini Bukoba, katika mkutano ambao pia umehudhuriwa na wawakilishi wa Shirika la Afya Duniani na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto.

Amesema hadi sasa idadi ya watu waliotengwa baada ya ndugu na jamaa zao wa karibu  kupoteza maisha kwa ugonjwa huo wanaoendelea kupata matibabu chini ya uangalizi maalum imefikia mia mbili na watano.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani(WHO), Bwana Zabuloni  Yoti na mwakilishi mkazi wa UNICEF, Shalini Bahunguna, wamepongeza hatua ya serikali za kudhibiti maambukizi hayo.