Back to top

‎TADB KINARA WA KUWEZESHA MIRADI YA UFUGAJI KUKU 

18 October 2026
Share

‎Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetunukiwa tuzo ya Taasisi ya Fedha Kinara katika Kuwezesha Miradi ya Ufugaji wa Kuku nchini, katika Maonesho ya 10 ya Ndege Wafugwao (Tanzania Poultry Show 2026).
‎
‎Tuzo hiyo imetolewa kutambua mchango wa TADB katika kuwawezesha wadau wa sekta ya ufugaji wa kuku kupitia huduma za kifedha zinazolenga kuongeza uzalishaji, kukuza biashara na kuchochea maendeleo ya uchumi wa Tanzania.
‎
‎Kupitia huduma zake za kifedha, TADB inaendelea kuwawezesha wakulima, wafugaji na wavuvi, sambamba na kuimarisha mnyororo wa thamani katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi ili kuchangia maendeleo endelevu nchini.
‎
‎Maonesho ya Tanzania Poultry Show 2026 yamefanyika Oktoba 16 na 17 katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.
‎
‎TADB inaendelea kusisitiza dhamira yake ya kuendeleza sekta ya kilimo nchini kupitia kaulimbiu yake isemayo: “TADB – Kilimo Kinabenkika.”