Back to top

Serikali yafuta ununuaji na uingizaji wa mbolea kwa njia ya Zabuni.

20 July 2021
Share

Waziri wa Kilimo Prof.Adolfu Mkenda amesema serikali imefuta mtindo wa ununuaji wa uingizaji wa mbolea hapa nchini kwa njia ya zabuni na badala yake ametoa fursa kwa wafanyabishara na wazalishaji wote wenye uwezo kuagiza na kuingiza mbolea hapa nchini bila vikwazo vyoyote baada ya bei ya mbolea kupanda kwa kiasi kikubwa katika soko la kimataifa na kusababisha uhaba mkubwa wa mbolea hapa nchini kwa sasa.

Waziri Mkenda ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea Bandari ya Dar es Salaam na kushuhudia shehena ya mbolea ambayo imeingizwa hapa nchini ikiwa ni mkakati wa serikali katika kuhakikisha mbolea inapatikana kwa wingi nchini na bei inashuka baada ya kupanda na upatikanaji wake kuwa mgumu.

Waziri Mkenda amesema kuwa serikali haina kodi kwenye mbolea ila sehemu pekee ya gharama ilikuwa ni ucheleweshaji wa kushusha mbolea pamoja na bei ya soko la dunia.

Kwa upande wake uongozi wa Bandari ukawatao hofu wakulima kuhusu ingiaji wa mbolea hapa nchini kutokana na kutegemea meli nyingi za mbolea kufika hapa nchini.