Back to top

Serikali yaifunga Shule ya Msingi Nyamkaz - Bukoba.

07 May 2021
Share

Serikali imeifunga kwa muda usiojulikana Shule ya Msingi  Nyamkazi iliyoko katika ya Manispaa ya Bukoba  baada ya kuzingirwa na maji yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwenye maeneo mbalimbali  mkoani Kagera na hivyo kusababishwa   mafuriko kutokana na ongezeko la maji katika  Ziwa Victoria. 

Uamzi wa kufunga shule umefanywa siku mbili baada ya  Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawiro kutoa mapendekezo kwa  madiwani ya kufanya mchakato kutafuta eneo jipya la ujenzi wa shule hiyo ili walinde usalama wa wanafunzi.