Back to top

Serikali yaingilia kati matukio ya moto shule za kiislam.

31 July 2020
Share

Kutokana na mfululizo wa matukio ya moto yaliyotokea katika taasisi za dini ya kislam ikiwamo Shule za Ilala Islamic na Kinondoni Muslim, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali kwa kushirikiana na vingozi wa dini hiyo tayari wameanza uchunguzi ili kuibaini chanzo cha tatizo hilo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Julai 31, 2020) wakati akishiriki swala na baraza la Eid el-Adh’haa iliyofanyika kitaifa jijini Dar es salaam.

Waziri Mkuu amewataka waislam kujiepusha kutoa matamko ya mtu mmoja mmoja yanayoweza kuwavuruga waislam wote bali waendeleze mshikamano na mahusiano kwa waislam wote na taasisi nyingine.

Naye, Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana amewataka watanzania kutambua kuwa uchaguzi mkuu ni wa watanzania wote, hivyo wanapaswa kuchagua viongozi wanaohitajika na ambao wataweza kukidhi haja za watanzania.