Back to top

Serikali yakiri kuwepo upungufu wa wafanyakazi wa sekta ya afya.

12 April 2018
Share

Serikali imesema inatambua kuwa kuna upungufu mkubwa wa wafanyakazi wa sekta ya afya mkoani Kigoma na kuwa jitihada za utatuzi wa hilo unaendelea.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe shimiwa JOSEPHAT KANDEGE amesema hayo Bungeni  Mjini Dodoma alipokuwa akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara hiyo.

Amesema katika Mkoa wa Kigoma mahitaji halisi ya wafanyakazi wa sekta ya afya ni  Elfu- 5 na Saba, na waliopo sasa ni 1,663 na kuwa Serikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha upungufu huo wa wafanyakazi unatatuliwa.

Majibu ya Naibu waziri huyo  wa TAMISEMI yalitokana na swali lililoulizwa na Mbunge   wa  Viti Maalum Mkoa wa Kigoma,Mhe shimiwa JOSEPHINE GENZABUKE kuhusiana na  mahitaji ya  watumishi wa sekta ya afya katika zahanati za Mkoa wa Kigoma.