Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema katika kuboresha huduma za hali ya hewa nchini Serikali imenunua rada tatu ambazo zitafungwa katika mikoa ya Mtwara, Mbeya na Kigoma.
Akizungumza jijini Dodoma ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya siku ya hali hewa Duniani katika ofisi za Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) Mhandisi Kamwelwe alisema, baada ya kufungwa rada hizo kutakuwa na mtandao wenye jumla ya Rada tano ambazo zitakuwa na uwezo wa kuliona anga la Tanzania kwa asilimia 70.