Back to top

Serikali yaokoa mabilioni ya fedha kutoka taasisi ya Masterlife.

06 April 2021
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Mwinyi amewahakishia wananchi kuwa serikali imechukua hatua za kuokoa fedha walizopoteza kupitia Taassi ya Masterlife, ambayo imedanganya watu na kujipatia Shilingi zaidi ya Bilioni 38.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Rais Mwinyi amesema taasisi hiyo iliyosajaliwa bara imedanganya kwa kutojishugulisha na biashara iliyosajaliwa ya kufuga wanyama na kuanza kujishugulisha na utoaji wa fedha na watu zaidi ya elfu 40 wametoa fedha wakitarajia faida.

Dk.Mwinyi amesema Serikali imeanza kuchukua hatua za kuzuia fedha kwenye benki mbalimbali, kuzuia magari na viwanja vya nyumba na fedha bilioni nne na uchunguzi unaendelea.

Wanannchi wengi walijitokeza kujiunga na taasisi hiyo ambayo imefungua matawi yake katika mikoa yote Unguja na Pemba ambao ilianza kutoa faida mwanzo ya aslimia 100 hali iliyowavutia watu wengi kujiunga na sasa wamejukuta fedha zao zimepotea.