Back to top

Serikali yaombwa kuanzisha mfuko maalum kusaidia wagonjwa wa TB.

08 August 2020
Share

Kutokana na idadi kubwa ya wananchi wanaobainika kuwa na Maambukizi ya Ugonjwa wa kifua kikuu kuwa na lishe duni katika maeneo mengi ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, serikali imeombwa kuanzisha mfuko maalumu kwa ajili ya kusaidia lishe kwa wagonjwa wenye maambukizi ya ugonjwa huo ili dawa wanazoanzishiwa ziweze kuwasaidia badala ya kuwaathiri zaidi.

Ombi hilo limetolewa na mganga mkuu wa hospitali ya misheni ya mbesa iliyopo katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Daktari Mzelifa Masaga wakati wa zoezi la upimaji wa ugonjwa wa kifua kikuu kwa watoto chini ya miaka mitano unaofanywa na kitengo cha kifua kikuu na ukoma kutoka hospitali ya wilaya ya Tunduru.

Naye Mratibu wa kitengo cha kifua kikuu na ukoma wilaya ya Tunduru, Daktari Mkasange Kihongole anawaonya wazazi wenye tabia ya kuwaachisha dawa za kifua kikuu watoto wao kwa makusudi kuacha tabia hiyo.

Bwana Ally Tarika mkazi wa Mbesa Tunduru anatoa ushuhuda wa kukaa mtoto wake nyumbani kwa kipindi kirefu bila kujua kama ana maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu.