Back to top

Serikali yaombwa kufuta mikataba mibovu katika sekta ya Kililmo.

15 January 2021
Share

Wakulima wadogo kutoka mikoa 6 inayozalisha chakula kwa wingi nchini wameiomba serikali kufuta mikataba yote mibovu ikiwemo ya kimataifa iliyoko kwenye sekta ya kilimo kwani athari zake kwa taifa ni kubwa kama zilizokuwa kwenye sekta ya madini.
 
Ombi hilo limetolewa leo jijini Arusha na wawakilishi wa wakulima hao walipokuwa wanazungumzia athari za tatizo hilo walilodai kuwa  ni kubwa zaidi kwenye uzalishaji wa mbegu.
 
Baadhi ya wakulima kutoka maeneo mbalimbali wameelezea baadhi ya mikataba inavyokwamisha ustawi wa kiilmo na pia baadhi ya mbegu zinazo wasababishia hasara.

Baadhi ya mikataba ya kimataifa inayodaiwa kuwaangamiza wakulima ni inayopendekezwa kufutwa ni pamoja na unaowakataza wakulima wadogo kuzalisha na kusambaza mbegu zao za asili kwa madai kuwa hazina sifa na zinatakiwa kutambuilwa kama nafaka suala ambalo wakulima hao  wanasema lina agenda iliyojificha.

Wakulima waliowasilisha pendekezo hilo ni wa mikoa ya Arusha, Morogoro na Kilimanjaro, Ruvuma na Kagera.