Back to top

SERIKALI YAONGEZA COMBINATION KUTOKA 16 HADI 65

20 March 2024
Share

Serikali imesema kuwa tayari imekamilisha zoezi la awali la uingizaji wa taarifa kwenye kanzidata (Database), zilizojazwa kwenye fomu za uchaguzi na wanafunzi wakati wakiwa shuleni.
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa OR-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, wakati akizungumza na vyombo vya habari, ambapo amebainisha kuwa mabadiliko ya sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014, Toleo la Mwaka 2023 na Mitaala ya Elimu kwa Kidato cha Tano yameanza kutekelezwa, ambapo utekelezaji huo umehusisha uanzishaji wa Tahasusi (Combination) mpya 49, kutoka 16 zilizokuwepo awali hadi kufikia tahasusi 65.