Back to top

Serikali yapokea msaada wa dawa na vifaa tiba.

14 January 2022
Share

Serikali kupitia Wizara ya Afya imepokea msaada wa dawa pamoja na vifaa tiba vyenye thamani ya Tsh Mil. 864 kutoka Serikali ya Misri vitavyosaidia kupambana dhidi ya magonjwa mbalimbali nchini.
.
Akipokea msaada huo, Prof. Makubi amebainisha kuwa, msaada huo unatokana na ziara ya kikazi ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan nchini Misri mnamo mwezi Novemba mwaka jana ambapo walikubaliana na Rais wa nchi hiyo Mh. Abdel Fattah Al-Sisi kukuza ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo afya.