Back to top

SERIKALI YARUHUSU DAGAA WALIOKWAMA KUSAFIRISHWA MARA.

03 February 2022
Share

Serikali imewaruhusu wafanyabiashara wa Dagaa Mkoani Mara waliokwama kwa zaidi ya siku 10 kusafirisha dagaa wao kwenda mikoa mingine kwa utaratibu wa kuwa na maafisa wa serikali katika magari yao huku Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi akiagizwa kuandaa utaratibu maalum utakaotumiwa na wafanyabiashara hao wanaosafirisha ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ametoa kauli hiyo alipotembelea eneo la Mwigobero lililopo mkoani humo ambalo ni lango kuu la wafanyabiashara hao kwa lengo la kuangalia magari yaliyokuwa na mizigo na kisha kutoa msimamo wa serikali.

Aidha, Waziri Ndaki amewataka Wafanyabiashara hao kuwa waaminifu ili serikali iweze kuwawekea mazingira mazuri ya kufanya biashara zao huku akiwaonya wale watakaokiuka taratibu watachukuliwa hatua ikiwemo kupigwa faini.

Wafanyabiashara hao wa Mazao ya Uvuvi walizuiwa kusafirisha Mazao yao tangu Januari 20 Mwaka huu  kwani baadhi yao wanatuhumiwa kutokuwa wakweli katika ufanyaji wa biashara zao na kusababisha serikali kukosa mapato yake.