Back to top

Serikali yasitisha uagizwaji mchele toka nje ya nchi ili kulinda soko

12 September 2018
Share

Serikali imesitisha uagizwaji wa mchele kutoka nje ya nchi ili kulinda masoko ya ndani kutokana na uwepo wa mchele wa kutosha zaidi ya tani milioni 2.2 wakati mahitaji halisi ya mchele ni tani laki 9.9

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi MATHEW MTIGUMWE ameyasema hayo  Mjini Moshi, alipokuwa akizungumza na wakulima wa mpunga kutoka mikoa mbalimbali inayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Japani - JAICA kupitia mradi wa kusaidia wakulima wa mpuga.

Amesema uzalishaji wa mchele hapa nchi kwa sasa umeongezeka kwa kasi baada ya wakulima kupatiwa mbinu bora za uzalishaji wa kilimo cha mpunga na kwamba mpaka sasa kuna ziada ya mchele Tani zaidi ya milioni Moja na Laki-mbili.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkuu wa JICA Bwana TOSHIO NAGASE amesema wakulima zaidi ya Elfu - 15 hapa nchini wamenufaika na mradi huo na kwamba tayari wakulima wamepata mafanikio makubwa kupitia kilimo cha mpunga.