Back to top

Serikali yasitisha ujenzi wa barabara ya Makongo-Goba

09 February 2020
Share

Serikali imesema imesitisha mpango wa kujenga barabara inayotoka Makongo kuelekea Goba na mkandarasi kuondoka katika  eneo hilo kutokana na hali ya mvua inayoendelea kunyesha katika maeneo mengi hapa nchini.

Akijibu swali la mbunge wa Kawe Mhe.Halima Mdee aliyeuliza ni lini serikali barabara inayotoka chuo cha ardhi kwenda Makongo hadi Goba itajengwa kwa kiwango cha lami na wananchi kulipwa fidia.

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasilianao Mhe.Isack Kamwelwe amekiri kuwa mkandarasi ameondoka katika eneo hilo kutokana na mvua zinazoendelea na kusisitiza kitaalamu kuwa barabara haziwezi kutengenezwa msimu wa mvua kutokana na hali ya udongo.