Back to top

Serikali yatahadharisha utapeli ajira za sensa.

28 March 2022
Share

Kufuatia taharuki iliyojitokeza nchini kuwa serikali imetangaza nafasi za ajira za makarani na wasimamizi wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 hatimaye Ofisi ya Taifa ya Takwimu imejitokeza hazarani na kukanusha taarifa hizo huku ikisisitiza kuwa haijatangaza nafasi zozote za ajira.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk Albina Chuwa ametoa tamko hilo jijini Dodoma ambapo amesema tayari Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imekwishatoa taarifa kwa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kuhusu tovuti ambayo imekuwa ikiwalaghai Watanzania kwa kutumia kivuli cha serikali.