Back to top

Serikali yatakiwa kumaliza migogoro ya ardhi inayotokana na mirathi.

04 July 2020
Share

KIGOMA.

Wananchi mkoani Kigoma, wameitaka serikali imalize migogoro ya ardhi inayotokana na mirathi, matumizi mabaya ya madaraka na utoaji wa hati miliki ya ardhi ya kiwanja kimoja kwa zaidi ya mtu mmoja, vitendo vinavyoathiri maendeleo.

Wakizungumza na ITV wakati wa ufunguzi wa ofisi ya ardhi ya mkoa wa Kigoma itakayokuwa ikitoa huduma za ardhi kwa wananchi, wamesema hatua hiyo itarahisisha utoaji wa haki na upatikanani wa nyaraka mbalimbali za umiliki wa ardhi.

Akifungua ofisi hiyo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi amewaagiza maofisa ardhi mkoani Kigoma kufanya kazi kwa haki na wasijihusishe na vitendo vya rushwa ambavyo vinawanyima haki wananchi.