
Serikali ya mkoa wa Mtwara imeigaza Bodi ya Korosho na Kamati ya pamoja ya ununuzi wa pembejeo, zihakikishe kampuni zilizoshinda zabuni ya ununuzi wa viuatilifu, magunia na mabomba msimu wa 2023-2024, inayogharimu zaidi ya shilingi bilioni 375 zinatekeleza mkataba uliosainiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbasi, ametoa agizo hilo wakati akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya ununuzi wa viwatilifu vya zao la Korosho kwa msimu wa mwka 2023-2024.
Ametaka mkataba huo uzingatiwe na mzabuni na atakayeshindwa kuutimiza aondolewe mara moja na aamriwe kulipa gharama za usumbufu na igawiwe kwa mzabuni mwingine.
Aidha, ameitaka Bodi ya Korosho ishirikiane na kamati ya ununuzi wa pamoja wa pembejeo, kusimamia mikataba ipasavyo ili zoezi hilo liweze kufanyika vema.
