Back to top

Serikali yatenga Bil. 100, Ujenzi Vyuo vya Ufundi Stadi

21 September 2022
Share

Waziri wa Elimu, Mhe.Prof. Adolf Mkenda amesema wana azma ya kujenga Vyuo vya Ufundi Stadi katika kila Mkoa na Wilaya nchini katika mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo amebainisha kuwa wametenga kiasi cha Shilingi Bil. 100 ili kuanza ujenzi wa vyuo hivyo kwenye Wilaya 62 ambazo hazina Vyuo hivyo. 
.
Waziri Mkenda ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe Dkt. Pius Stephen Chaya, Mbunge wa Jimbo Manyoni Mashariki aliyetaka kufahamu serikali ina Mpango gani wa kujenga Chuo cha VETA Wilayani Manyoni.