Back to top

Serikali yatoa bilioni 4 kuboresha miundombinu ya maji.

24 September 2020
Share

Serikali imetoa shilingi bilioni 4 kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Mtwara za kuboresha miundombinu ya maji, ili kuongeza kiasi cha maji kwa wakazi wa mji wa Mtwara na wawekezaji.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo Mhandishi Festo Fulgensi amesema hayo mbele ya Mkurugenzi wa Ubora wa Maji na Maabara wa Wizara ya Maji Mhandisi Phillipo Chambi.

Akizungumza baada ya kukagua miradi ya maji mkoani humo Mkurugenzi wa Ubora wa Maji na Maabara wa Wizara ya Maji Mhandisi Phillipo Chambi ameagiza miradi yote ya maji ikamilishwe kwa wakati.