Back to top

SERIKALI YAWAASA MAKANDARASI KUJIUNGA ILI KUONGEZA NGUVU KUTEKELEZA MI

26 May 2023
Share

Serikali imetoa rai kwa makandarasi wa ndani kujiunga ili kuongeza nguvu katika kutekeleza miradi pamoja na kutumia wataalam wenye sifa ili wawezekuamininiwa na serikali pamoja na mataifa mengine  ili kuongeza pato la taifa kupitia utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya katika ufunguzi wa mkutano wa wadau wa sekta ya ujenzi ulioandaliwa na bodi ya usajili wa makandarasi (CRB) mkoani Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi Mhandisi Joseph Nyamhanga ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fursa kwa Makandarasi wa ndani na kuwataka Makandarasi wazawa kufanya kazi kwa weledi.

Akiwasilisha mapendekezo ya wadau wa ujenzi kupitia mkutano huo, Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi mhandisi Rhoben Nkori amesema ili kuinua sekta ya Makandarasi nchini ipo haja ya sheria kuweka upendeleo kwa wazawa.