Back to top

Serikali yaweka tahadhari kudhibiti Ebola.

21 August 2018
Share

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Mh.Ummy Mwalimu amesema serikali imeongeza tahadhari ya hali ya juu kufuatia kuongezeka kwa wagonjwa wanaougua Ebola katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya CONGO.

Akiongea leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mh.Ummy amesema shirika la afya duniani (WHO) limefanya tathimini ya hatari ya kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola nchini DRC na nchi zinazopakana na DRC.

Katika mkutano uliohudhuriwa na Naibu Waziri wa Afya na mganga mkuu wa serikali, waziri ummy amesema WHO imebaini kwamba hatari ya kusambaa kwa ugonjwa huo kwa nchi jirani na DRC ikiwamo Tanzania imeongezeka maradufu.