Back to top

SHABIKI WA SIMBA AKAMATWA KWA KUHAMASISHA VURUGU

19 April 2024
Share

Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata Abdulshahib Hegga, maarufu kwa jina la @official_gb64, kwenye mtandao wa Instagram, kwa tuhuma za kuhamasisha watu kufanya vurugu katika mchezo wa watani wa jadi, Yanga na Simba, unaotarajiwa kuchezwa hapo kesho Aprili 20, 2024, katika Dimba la Mkapa.
.
Jeshi hilo limetoa taarifa hiyo kupitia mitandao yake ya kijamii ambapo limesema, mtuhumiwa huyo, alitoa hamasa hizo kupitia kipande cha video alichokisambaza kwenye mitandao ya kijamii na kwamba anaendelea kuhojiwa kwa kina.
.
Aidha Jeshi hilo limesema limejipanga na limechukua tahadhari zote za kiusalama kuelekea mchezo huo, ambapo limetoa tahadhari kwa mashabiki wote watakaoanzisha vurugu zozote au kujihusisha na vitendo vya kihalifu ndani au nje ya uwanja watashughulikiwa haraka kwa mujibu wa sheria.