
#HABARI: Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imeendelea kusikiliza Ushahidi katika kesi ya Uhaini ya Lissu, ambapo shahidi wa kwanza anaelindwa P2 (38) ambae ni fundi umeme ameshatoa ushahidi wake akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Igras Mwinuka.
Ameieleza Mahakama kuwa yeye ni mfuasi wa CHADEMA kuanzia 2021 na alianza kujishughulisha kwenye mikutano na michango ya mikutano tonetone.
Anaeleza kuwa Aprili 4, 2025 alikuwa kwenye shughuli zake Songea anakumbuka kipindi anapitia mtandao wa kijamii alikutana na video ya Lissu, ambapo alikuwa na mkutano Dar es Salaam.
Akiwa kwenye mtandao wa kijamii wa YouTube wakati anaperuzi akakutana na ujumbe wa Mwenyekiti wa chama akiwalekeza kuwa Mwaka huu (mwaka jana 2025) hakutakuwa na uchaguzi, kwa wale ambao wanataka kugombea udiwani, ubunge na Urais wasahau.
Akamtafuta Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Essau Chiza, ili kupata ufafanuzi anasema ilipofika Aprili 4, 2025 akatafutwa na kuambiwa kuna ziara ya Lissu itafanyika mkoa wa Ruvuma watoe mchango wa hiyari tone tone ambapo yeye akatoa 10,000 ili kuwezesha ziara.
Anaeleza waliambiwa mkutano utafanyika Aprili 10, 2025 saa nne asubuhi akaendelea na shughuli zake akisubiri hiyo siku. Ilipofika Aprili 9, 2025 akifuatilia taarifa za habari kwenye mitandao ya kijamii, akapata taarifa za kuwa Lissu amekamatwa anadai hakuwa na taarifa za kutosha ilipofika Aprili 10, 2025 akajiandaa kwenda kwenye mkutano kupata taarifa zaidi.
Alipofika uwanjani akakuta magari ya polisi akakuta taarifa za kuwa hakutakuwa na mkutano ndipo akatoka kwenda mjini kwenye ofisi za CHADEMA eneo la Mfaranyaki mchana. Wanachama wengine wa CHADEMA wakawa wanasema Heche ataongea akawa anasibiri kupata ufafanuzi kwa nini mkutano haujfanyika na kwa nini Mwenyekiti amekamatwa.
Kipindi anaelekea huko alipofika akakuta viongozi wa Mkoa, Heche, Lema na wengine kabla hawajaongea na waandishi yakaja magari ya polisi na kuwaambia wapo chini ya ulinzi akajikuta amekamatwa na kupelekwa Polisi kwa RPC.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
