Back to top

SHAMBULIO MOSCOW, PUTIN ACHARUKA, ISIS WAJITAJA.

23 March 2024
Share

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa hotuba yake kwa umma, akilitaja shambulio la Moscow kuwa ni kitendo cha kigaidi na kuahidi kuwaadhibu wahusika huku akiishutumu Ukraine kwa kusaidia washukiwa kutoroka hata hivyo Kyiv imekanusha vikali kuhusika na shambulio hilo.

Urusi imewakamata watu 11, wakiwemo watu 4 wenye silaha wanaoshukiwa kufanya shambulizi katika ukumbi wa tamasha uliojaa watu katika kitongoji cha Moscow jana usiku.

Takriban watu 133 wameuawa huku miili zaidi ikipatikana kwenye vifusi, Kamati ya Uchunguzi ya Urusi ilisema asubuhi ya leo huku idadi ya vifo ikitarajiwa kuongezeka.

Wanaume waliokuwa wamejificha waliingia ndani ya jumba la tamasha, wakafyatua risasi na kuuchoma moto ukumbi huo.
 
Kundi la kigaidi la ISIS limedai kuhusika lakini halikutoa uthibitisho wa madai hayo.
NBC NEWS