Back to top

Shein ongoza wananchi katika kisomo maalum kumuombea Marehemu Karume.

07 April 2018
Share

Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Ali Mohamed Shein amewaongoza mamia ya wananchi katika kisomo maalum cha hitima kwa ajili ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu mzee Abeid Karume huku akiwakemea wale wanaobeza uwepo wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

Dkt. Shein ametoa tahadhari hiyo wakati akizumgumza na ITV mara baada ya kushiriki hitima hiyo iliyohudhuriwa na viongzoi mblimbali wa juu wa serikali zote mbili akiwmeo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na, marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Dkt. Amani Abeid Karume na familia ya marehemu ikiongozwa na mjane Mama Fatma Karume ambapo Dkt. Shein amesema jina la serikali ya mapinduzi litabaki na halitaondoshwa.

Huku mvua ikinyesha ITV ilipata fursa ya kuongea na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye amesema watanzania mpaka sasa wanafaidika naye Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt.Amani Abeid Karume naye alitaka wananchi kuweka umuhimu wa historai, Huku  mjane wa Marehehu Mama Fatma Karume ameitaka serilai imuenzi mzee Karume kwa vitendo.

Katika siku hiyo maalum ya miaka 46 ya kumbukumbu ya mzee Karume viongzi wa dini walimuombea Marehemu mzee Karume na Dkt. Shein aliwaongoza viongozi wengine kuweka mashada ya maua akiwemo mwaklishi wa mkuu wa majeshi, Mabalzoi wa nje na familia ikiwa ni kumbukumbu ya siku hiyo kwa wananchi wa Zanzibar kwa mzee Karume Rais ambaye aliweka misingi imara ya uongzoi na uadilifu.