
Uongozi wa Mahakama ya Tanzania umetoa taarifa ya kuwajulisha wadau wake na wananchi kwa ujumla kuwa sherehe za Siku ya Sheria zilizokuwa zifanyike februari 01, 2022 zimeahirishwa kutokana na sababu zisizozuilika na badala yake zitafanyika siku ya jumatano februari 02, 2022 katika Uwanja wa Chinangali Jijini Dodoma ambapo Mh.Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

