Back to top

Sherehe ya kuzaliwa Mtume Muhammad kufanyika Usiku wa Oktoba 28.

20 October 2020
Share


Waislam nchini wanatarajia kuungana na Waislam wengine Duniani, katika kusherekea siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad, Rehema na Amani ziwe juu yake, zitakazofanyika usiku wa tarehe 28 mwezi huu.

Maulid kitaifa yanatarajiwa kusomwa usiku baada ya watu kupiga kura na yatasomwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja na Mufti wa Tanzania,  Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo.

Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally

Akizungumza kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislam pamoja na Mufti wa Tanzania, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum  amesema Mkoa wa Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa sherehe hizo za Maulid.

Sheikh huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema kwa vile mchana wa tarehe 28 ambayo ni siku ya maulid inaambatana uchaguzi mkuu, hakutakuwa na maandamano au Zafa kama ilivyozoeleka kwa siku za nyuma.

Sheikh Alhad Mussa Salum amesema Baraza la Maulid litafanyika tare he 29 katika viwanja vya Karimjee na Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa baraza hilo.