Back to top

Sheria 78 zimetungwa tangu kuanzishwa kwa Bunge la Afrika Mashariki.

16 May 2018
Share

Serikali imesema tangu kuanzishwa kwa Bunge la Afrika Mashariki mwaka 2001 hadi sasa jumla ya sheria 78 zimetungwa na kati ya hizo sheria 20 zimeridhiwa na wakuu wa nchi wanachama huku nyingine zikiwa zipo katika hatua mbalimbali za kusainiwa na kuridhiwa.
 
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mh Dk. Augustine Mahiga wakati akijibu swali la Mh Ally Salehe Mbunge wa Malindi aliyetaka kujua ni sheria ngapi zimetungwa tangu kuanzishwa kwa umoja huo.
 
Mh dk. Mahiga amesema sheria zilizotungwa zimelenga katika kuimarisha biashara kukuza uchumi baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuwezesha taasisi na vyombo vya jumuiya kutekeleza majukumu yake.